Habari za Bonyad

Kufanyika Majilisi ya Shahada ya Imam kadhim (a.s) na Kumbukumbu ya kifo cha Marhum Sayyid Murtadha Rizvi (r.a) katika Ofisi ya Buniyad Akhtar Taban

Majilisi ya Shahada ya Imam kadhim ilifanyika Katika siku  ya Shahada ya  Imam kadhim (a.s) na Kumbukumbu ya kifo cha Marhum Sayyid Murtadha Rizvi (r.a). Majilisi hii ilifanyika katika Ofisi ya  Buniyad Akhtar Taban ilioko karibu na Haram ya bibi Fatmah  Ma’sumah (a.s) katika mji mtukufu wa Qom katika usiku wa Shahada ya Imam Kadhim (a.s). 
Vile vile ilifanyika majilisi ya kisomo cha kukhitimisha Qur’an kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kifo cha Marhum Sayyid Murtadha(r.a)  Mtoto wa Marhum  Allamah Sayyid Saed Akhtar Rizvi katika ukumbi wa Buniyad Akhtar Taban.
Katika majilisi hii walihudhuria wageni  kutota mataifa ya Afrika mashariki na India.
Majilisi hii ilianza kwa kisomo cha Qur’an kilichosomwa na Syed Muhmmad Jayydi  na iliendelea kwa nauha kutoka kwa Syed Hassan  Miry Yazdi na Khutba ya Hujjatul-Islam wal muslimin Syed Kalb Hasan mmoja kati ya Maulamaa wa India  na Hujjatul-Islam wal muslimin Dk Jahangiry   Naibu wa Kimataifa wa Chuo cha Adiyan wamadhahib.
Na mwishoni mwa majilisi hii wageni wote  walikaribishwa katika karamu ya Imam Kadhim (a.s).

Leave a Reply

Back to top button
×