Aamal na DuaBONYAD AKHTAR TABANELIMU YA KIISLAMUHabari za BonyadMatukio ya Kiislamu

Kufunga funga sahihi na ya kweli

Nikitanguliza pongezi kwa kuwasili / kuingia kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ningependa leo hii mimi pamoja nanyi tutizame na tupitie Dua ya siku ya kwanza ya Ramadhan:

Katika Dua ya Siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, mja huomba maombi makuu 5 kutoka kwa Mwenyezi Mungu(swt):

1- Kufunga funga sahihi na ya kweli.
2- Kufanikiwa kusimama usiku kwa ajili ya kufanya ibada za usiku.
3- Kuamka kutoka katika kughafilika.
4- Kuepuka kufanya uovu, uhalifu na kutenda dhambi.
5- Kuomba Msamaha na Maghfira kwa dhambi na makosa tuliyoyatanguliza.

Hebu tusome na turudie kwa Dua hii ya Siku ya Kwanza kwa pamoja:

“Ee Mwenyezi Mungu, ifanye Funga yangu katika siku hii ya leo kuwa funga sawa na ile funga ya waja wako waliofunga sawasawa na saumu ya kweli na ikhlasi. Na jalia kusimama kwangu katika sala na ibada kuwe kama kusimama kwa wale wanaosimama katika ibada kwa utiifu. Niamshe / nizindue ndani yake nitoke katika usingizi wa walioghafilika, na unighufirie madhambi yangu. Ewe Mola wa Walimwengu! Nisamehe. Ewe mwenye kuwasamehe wakosefu.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button
×