Habari

Majlis ya maombolezo ya Maulla Al-Muwahhidin ilifanywa na Bonyad Akhtar Taban katika Husseiniyah ya Imam Swadiq (a.s)

Majlis ya kuomboleza shahada ya Maulla Al-Muwahhidin Amir al-Mu’minin Ali (as) iliyohudhuriwa na wafuasi na wapenzi wa kizazi cha Mtume kitoharifu (as), na ilifanyika kwa kuchunga kanuni za Afya ndani ya Husseiniyah ya Imam Swadiq (as) karibu na Haram ya Bibi Fatwimatul-Maasuma (as).
Majlis hiyo iliandaliwa na Bonyad Akhtar Taban na ilihudhuriwa na Mashia wa Amir al-Mu’minin (as) wanaozungumza Kiurdu wa kutoka nchini India na Pakistan.
Majlisi hiyo ilianza kwa kisomo cha Qur’ani Tukufu, na kisha Washairi na wasifu wa Ahlul-Bayt (as) waliwasilisha mashairi yao kwaajili ya kumsifu Ali (as).
Khatibu wa Majlis hiyo alikuwa ni Hujjatul-Islam wal-Muslimini, Sayyed Sibtwain Abbas Rizvi, miongoni mwa Makhatibu na walimu wa Hawza.
Majlisi hiyo ilimalizika kwa maombolezo na Nawha za shahada ya Imam Ali.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button
× Whatsapp Support