Habari

Ziarah Kwa Mashahidi wa Uhud

Mtindo wa Maisha ya Hazrat Fatima Zahara (sa) (3)

   Sayyidat Fatima (sa) akiwa amekatishwa tamaa ya watu waliomzunguka, anakaa karibu na makaburi ya mashahidi na anautazama Mlima wa Uhud.

   Anakumbuka kwamba Waislamu walitelekeza korongo (la mlima) kando ya mlima huu kwa sababu ya tamaa ya ngawira, na hilo likasababisha kushindwa (kwao katika vita).

   Wakati huo, alikumbuka kipindi hicho cha vita ya Uhud pindi  alipofika katika sehemu hiyo ili kuwahudumia majeruhi, kwa sababu alikuwa akiamini kwamba inapobidi, wanawake wanapaswa pia kuhudhuria (na kuonyesha uwepo wao) katika Jamii ili kuilinda dini ya Mwenyezi Mungu.

   Hazrat Fatima (sa) kama ilivyokuwa baada ya kufariki kwa baba yake, alisimama pia imara ili kumhami na kumtetea Kiongozi wake, yaani mume wake Imam Ali (as), kwa sababu watu wengi walimuacha Hoja na Walii wa Mwenyezi Mungu peke yake (nyuma yake kukiwa ni patupu) kwa sababu ya tamaa na uroho wa ngawira.

    Majo ya malengo ya HZazrat Fatima al- Zahra(sa) katika kuwazuru (kuwatembelea) Mashahidi wa Uhud, hasa Sayyid Al-Shuhadaa Hazrat Hamza (ra), labda ilikuwa ni kutaka kuwaonyesha watu kwamba Hazrat Hamza (ra) alikuwa Mwenye kuihami Familia ya Mtume Muhammad(saww), na kama angelikuwa hai, basi kwa hakika hali ingelikuwa tofauti na leo.

(Sharh Nahj al-Balagha, Juz.15, Uk.35- Al-Kafi Sheikh Kilini, Juz. 3, uk. 228. Bihar Al-Anwar, Juz. 38, uk. 202- Seerah Ibn Hisham, Juz. 3, uk. 106.)

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button
×