Hafla Ya Kumalizika Kwa Kozi Ya Kwanza Ya Kumlea Mubaligh

Kikao hiki kilifanyika pamoja na mnasaba wa kuzaliwa Muokozi wa Wanadamu Almahd (aj) katika Ofisi ya Buniyad Akhtar Taban.
Khutba maalum ya kikao hiki ilitolewa na Mkuu wa Televisheni ya Waliyul-A’sir(aj) Ayatu Allah Husseini Qaziwini (Mwenyezi Mungu ampe umri mrefu).
Kikao hiki kilihudhuria na Wageni mbali mbali kutoka Nchi tofauti tofauti mingoni mwazo ni India na Nchi za Afrika Mashariki
Ayatu Allah Husseini Qaziwini alizungumzia nukta muhimu za mafanikio ya Kitablighi.
Mwishoni wa kikao hiki Washiriki wa kozi hii walikabidhiwa Shahada na Ayatu Allah Husseini Qaziwini na wakapiga picha ya Pamoja.
Na pia alikuwa na mazungumzo haswa pamoja na Mkuu wa Buniyad Akhtar Taban Hujjatul-Islam wal muslimin Sayyid Kadhim Rizvi ambapo alipongeza harakati za Buniyad Akhtar Taban na alionesha utayari wake wa kushirikiana katika kozi za kuufahamu Ushia na kujibu Shubuhati za Mawahabi.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button
×