Habari

Kumbukumbu ya kifo cha Abu Ja’far Musa bin Muhammad al-Mubarqa(as)

Hadhrat Musa Al-Mubarqaa (as) alifariki Tarehe 22 au 28 Rabiul Awwal, Mwaka 296 Hijria, katika Mji wa Qom, na alizikwa katika linaloitwa: Chehel Akhtaran

Abu Ja’far Musa bin Muhammad al-Mubarqa alikuwa mtoto wa Imamu wa 9 wa Shia Ithna Ashari (Imamiyyah) Muhammad Jawad, na kaka mdogo wa Imam wa 10, Ali Al-Hadi(as).

Anajulikana zaidi kama babu wa Masayyid wote wanaotumia Jina la Babu yake, Imam wa 8, Ali al-Ridha (a.s) kama jina lao la ukoo.

Wengi wa Masayyid wanaoitwa ‘Rizvi’ (au ‘Radhawiy’ au ‘Razavi’) ni katika Kizazi cha Musa al-Mubarqa.

Wengi wao walipatikana Sabzevar, Iran, kabla ya kuhamia Bara Hindi.

Bado kuna vijiji na miji michache nchini India ambayo kunapatikana ukoo huu wa ‘Rizvi’ ambao unarudi hadi kwa Hazrat Musa al-Mubarqa kupitia kwa mtoto wake Shahzada (Mfalme) Ahmad bin Musa.

Musa al-Mubarqa alikuwa ni miongoni mwa Wacha Mungu na wapole na wapokezi maarufu wa Riwaya katika zama zake, na mapokezi mengi kupitia kwake yamenukuliwa na kusajiriwa katika vitabu mbalimbali vya Hadithi, ambapo ni pamoja na kitabu maarufu kinachoitwa “Tuhaf al-Uqul”.

Hadhrat Musa Al-Mubarqaa (as) alifariki Tarehe 22 au 28 Rabiul Awwal, Mwaka 296 Hijria, katika Mji wa Qom, na alizikwa katika linaloitwa: Chehel Akhtaran.

Related Articles

Leave a Reply

Check Also
Close
Back to top button
×