Habari

Kufanyika kwa kumbukumbu ya kumi na tisa ya kifo cha Raisul Muballeghin Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (r.a)

Kikao hiki cha kumbukumbu ya kifo cha Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (r.a) kilifanyika Mji mtukufu wa Qom katika siku aliokufa, chini ya usimamizi wa Ofisi ya Bonyad Akhtar Taban.
Katika kikao hiki ambacho kilifanyika katika Shule ya Aalul-Bayt (a.s) kilihudhuriwa na Maulamaa na Wanafunzi kutoka nchi za Afrika na pia nchi za Ghuba ya Uajemi na India.
Baada ya kisomo cha Qur’an tukufu kilichosomwa na Maustadh wa Qur’an, Hujjatul-Islam wal-Muslimen Sheikh Abdul-Majid mmoja wa Maulamaa wa Afrika Mashariki ambae kwa miaka mingi alikuwa pamoja na Allama (r.a) aliezea na kufafanua kuhusu maisha ya Allama (r.a) na huduma alizozitoa katika uhai wake.
Katika kikao hiki khutuba ilitolewa na Ayatullah Sayyid A’dil Alawy (M.Mungu amuhifadhi) mmoja wa Maustadh na Khatib wa Hawza ya Qom na Najaf.
Katika khutba yake alizungumzia na kubainisha daraja la A’lim na Tabligh katika hadith za Kiislam na kutukuza daraja la elimu na Shakhsia ya Allamah (r.a).
Kikao hiki kilihitimishwa kwa nauha ya kukumbuka mateso ya Ahlul-Bayt iliosomwa na Mh’ Dhwaighamy.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button
×