Habarinyumba ya sanaa ya picha

Nimepata Nuru ya Ukweli na Uhakika kupitia vitabu vya Allamah Sayyid Saed Akhtar Rizvi(ra)

Katika makala hii, anasimulia mmoja wa Mashia wa nchi Rwanda, Mkazi wa Jiji la Kigali, ambaye alisoma vitabu vya Allamah Syed Saeed Akhtar Rizvi(ra) na kupitia vitabu hivyo akaipata Nuru ya Ahlul-Bayt(as), na akawa mfuasi wa Maimam Watukufu wa Nyumba Tukufu ya Mtume Muhammad (saw). Kuhusu anaandika kama ifuatavyo

Assalam Alaykum wa Rahmatullah wa Barakatuh.

Bismillah Rahman Rahim.

Allahuma Sali alaa Muhammad wa Aali Muhammad.

Kwa jina naitwa: Jamaal Rangira. Mkazi wa Kigali, nchini Rwanda.

Binafsi hapo awali nilikuwa mfuasi wa Madhehebu ya Sunni kabla ya kugeuka na kuwa mfuasi wa Madhehebu ya Shia Ithna Asharia.

Niliamua kuwa mfuasi wa Madhehebu ya Shia Ithna Asharia kutokana na kusoma kwa wingi vitabu vya Marhumu Allamah Sayyid Saed Akhtar Rizvi (ra) ambavyo nilibarikiwa kuvipata na kuvisoma kwa umakini katika harakati yangu ya kutafuta ukweli na uhakika.

Vitabu vyake vilikuwa ma hoja imara zaidi na zenye kukinaisha. Viliweza kunipa mwanga na kuniwezesha kuelewa, kufahamu na kubaini  usahihi na ukweli wa Madhehebu ya watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume Muhammad (saww).

Miongoni mwa vitabu vyake ambavyo vilinishawishi kufuata Madhehebu ya Shia Ithna Asharia, ni vitabu kama vile:

1-Maana na chanzo cha ushia.

2-Qur’an na Hadith.

3-Muhammad (saww) ni Nabii wa mwisho.

Kwa hakika vitabu hivi vilinisaidia sana kuelewa mambo mengi ambayo sikuwa ni mwenye kuyafahamu nilipokuwa katika Usunni.

Leo hii mimi ni mfuasi wa Ahlul Bayt(as) ambaye nimeujua ukweli na Uislamu halisi wa Mtume wetu Muhammad(saww) kupitia vitabu hivyo vya Allamah Rizvi(ra).

Ukweli ni kwamba: Sisi Mashia wa Rwanda tumefaidika sana na harakati ya Kitabligh ya Sayyid  Saed Akhtar Rizvi(ra).

Hakuna Mshia wa nchi ya Rwanda ambaye hajasoma vitabu vyake.

Tunamuombea Sayyid Mwema Allah (swt) amjalie Pepo ya Firdaus, kutokana na kazi kubwa ya Tabligh aliyoifanya Afrika Mashariki kwa kuwaongoza vyema watu ili kujua haki na ukweli wa Madhehebu ya Ahlul Bayt (as).

Vitabu vyake vilichangia kwa kiasi kikubwa kueneza Ushia huku kwetu Rwanda na hata nchi zingine za Afrika Mashariki na kati.

Ushauri wangu:

Nawausia waislamu wenzangu kusoma Zaidi vitabu vya Allamah Rizvi(ra), kwa hakika vimejaa Ukweli, Usahihi na Uislamu wa Haki.

Wabillah Tawfiq.

Jamaal Rangira.

Rwanda, Kigali.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button
×