Habari

MWONGOZO WA IMAM MUSSA AL-KADHIM (A.S)

Mashia wanapaswa kukabiliana vipi na serikali dhalimu?

MWONGOZO WA IMAM MUSSA AL-KADHIM (A.S)

Funzo kutoka katika mwongozo wa Imamu Kazim (a.s):

Je, Mashia wanapaswa kukabiliana vipi na serikali dhalimu?.

Zama za Hadhrat Imam Musa al-Kazim (a.s) zilikuwa za kisiasa sana na watawala wa wakati huo hawakuacha fursa yoyote ya kuwasumbua na kuwanyanyasa Mashia pamoja na Imam wao Musa al-Kazim (a.s), hata hivyo, siku zote Imam Musa (a.s) alisimamia na kuongoza vizuri jamii yake, na aliwafunza na kuwaelezea ni jinsi gani ya kuhifadhi mstari mwekundu wa kidini na kukabiliana au kupigana dhidi ya watawala madhalimu na wanyakuzi wa haki za watu.
Swali la msingi lilikuwa: Ni jinsi gani ya kukabiliana na watawala madhalimu au Serikali dhalimu?!

Jibu la swali hili linaweza kupatikana katika yale mapendekezo, nasaha, na msisitizo wa Imamu Kazim (a.s) kwa Saf’wan bin Mehran Jammal:

Alipopewa heshima kama Mshia ya kumtumikia Imamu Kazim (a.s) kama Mshia, alimwambia:

«یَا صَفْوَانُ کُلُّ شَیْ‌ءٍ مِنْكَ حَسَنٌ جَمِیلٌ مَا خَلَا شَیْئاً وَاحِداً»

“Ewe Saf’wan, kila kitu chako ni kizuri, ispokuwa kitu kimoja tu”

Saf’wan akauliza: Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hicho ni kitu (au jambo) gani?.

Imam akasema:

“Utawakodisha Ngamia wako kwa mtu huyu – yaani, Harun -“

Safwan akasema:
Mimi siwakodishi Ngamia wangu kwake kwa ajili ya upuuzi wa anasa na kuwinda na mengineyo, bali nafanya hivyo kwa ajili ya safari ya Hajj tu.

Katika suala hii, yeye (Harun) hahusiki nalo mwenyewe moja kwa moja, badala yake, yeye huajiri wengine wafanye kwa ajili yake.

Imam Musa Al-Kadhim (a.s) akasema:

“Ewe Saf’wan, je, unadhani ni sahihi kwako wewe kuwakodisha wao Ngamia wako?!.

Saf’wan akasema: Ndio.

Imam (as) akasema:
Je, unataka waendelee kuishi hadi kumalizika muda wa kukodishwa Ngamia wako, na kurudishiwa kwa Ngamia wako na malipo yako?.

Saf’wan akasema: Ndiyo.

Imam (a.s) akasema:

“Mtu yeyote anayependa waendelee kuishi, huyo ni mmoja wao, na anakuwa katika safu miongoni mwao, na yeyote awaye miongoni mwao, ataingia katika moto wa Jahannam”.

Baada ya hapo, Saf’wan aliuza ngamia wake wote na Harun alipouliza sababu ya hili, alijibiwa hivi:

“Mimi ni mzee sasa, na vijana wangu hawawezi tena kufanya hii kazi ya kuwatunza Ngamia hao inavyopaswa.

Harun akasema:
Najua ni nani uliyekushauri wewe kuuza Ngamia wako; ni Musa bin Jafar aliyekufanya ufanye hivi.

Akasema: Nimefanya nini mimi – au nina kazi gani mimi – na huyo Musa bin Jafar?!.

Haroun akasema: “Achana na hilo, lakini nakuapia kwa Mwenyezi Mungu lau kama sio wema wako na usuhuba wako mzuri kwangu; ningelikuua”.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button
×