Habari

Zawadi ya Kujibu Maswali

Mtindo wa Maisha ya Hazrat Fatima Zahra sa (6)

Imamu Hasan Askari (as) alisema:

Siku moja, mwanamke mmoja alikuja kwa Hadhrat Fatima Zahra (sa) na akasema: Nina mama ambaye ni dhaifu na asiye na uwezo wa kuswali, amenituma nije kwako nipate kuhusiana na masiala hii.

Baada ya kusikiliza maelezo ya mwanamke huyo, Hadhrat Zahra (sa) alimpatia jibu lake, na mwanamke huyo akarudia swali lake kwa mara pili, na Hadhrat akamjibu tena kwa mara ya pili.

Mwanamke huyo kama kawaida alirudia swali lake mara kwa mara mpaka ilipofikia mara kumi, na Hadhrat Zahra (sa) akamjibu bila ya hisia yoyote au kudhihirisha kuwa amesumbuliwa, bali alimjibu kwa upole na huruma.

Baada ya hapo, mwanamke huyo aliona aibu na kusema: Nimekuchosha na kukusumbua, sitakusumbua tena.

Hadhrat Zahra (sa) akasema: Hapana, haitakuwa shida wala usumbufu  kwangu, kisha akaongeza: Ni kama vile mtu ikiwa ataajiriwa kubeba mzigo mkubwa na kuupeleka mahali fulani, na akapokea ujira wa dinari laki moja kwa kazi hiyo, je! Atahisi shida na usumbufu?!.

Mwanamke yule akajibu kwa kusema: Hapana.

Baada ya hayo Hadhrat Fatima (sa) akasema: Mimi ni muajiriwa wako kwa kila swali ninalojibu, na malipo yake yana thamani kubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko yale yote yaliyomo duniani.

Basi, uliza chochote unachotaka kuuliza na kwangu sio sababu ya usumbufu, kama nilivyosikia kutoka kwa baba yangu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akisema:

Maulamaa na Wanachuoni, Mashia na wafuasi wetu watakusanywa pamoja Siku ya Kiyama wakati wa ufufuo, wakiwa wamevaa taji la utukufu.

Kwa sababu hao wamejitahidi sana kuwaongoza waja wa Mwenyezi Mungu katika ulimwengu huu, hivyo watapata neema na rehema za Mwenyezi Mungu, na watakabidhiwa zawadi na mavazi ya thamani zaidi Peponi…

Baada ya hapo, Hadhrat Zahra (sa) akasema: Ewe mja wa Mwenyezi Mungu! Thamani ya moja ya mavazi hayo ya Peponi, ni mara elfu zaidi ya yale yaliyopo katika dunia hii na na yakimulikwa na jua.

Kwa sababu mambo ya dunia hii, ingawa yanaonekana katika dhahiri kuwa na thamani kubwa; lakini kwa hakika ni mambo yanayoharibika na kutoweka, hii ni tofauti na siku ya Kiyama na Peponi, ambapo kila kitu kilichopo ndani yake kitakuwa salama na kitadumu milele.

(Tafseer al-Imam al-Askari(as), Uk. 340, Hadithi 216, Biharul-An’war: Juzuu ya 2, Uk.3, Hadithi 30.(

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button
×