Habari

Khutba ya Fatima Msikitini

Mtindo wa Maisha ya Hazrat Fatima Zahra sa (2)

Hadhrat Fatima Zahra (sa) anakwenda Msikitini, ambapo anaomboleza akiwa na machungu moyoni, na kila mtu anaanza kulia.

Muda mfupi baadaye anatulia, na kusubiria kidogo kwa muda ili kuruhusu (kilio au) kishindo cha umati kitulie.

Kisha anatoa khutba ndefu kuhusu mafundisho ya dini na kuthibitisha haki yake iliyonyakuliwa (na kuporwa) akitumia Aya Tukufu, Riwaya na na dalili za kimantiki, na hotuba hiyo inajulikana kama “Hotuba ya Fadak”.

Katika hotuba hii:
Anaanza kwa kumhimidi Mwenyezi Mungu na kumsalia Mtume (saww).

Khutba hii ya Fadak inajumuisha mafundisho ya kina ya Mwenyezi Mungu, hadithi ya hikaya juu ya ukandamizaji wa familia ya Mtume (saww) na ulinzi wa adhama na heshima ya Wilayat.

Khutba hii ina rangi na ladha ya wahyi ambapo Hadhrat Zahra (sa) kupitia khutba hiyo anatimiza ushahidi (uthibitisho) na dalili kwa kila mtu na anaondoka zake Msikitini.

Hotuba ya Fadak inapaswa kusomwa kwa uangalifu na tunapaswa kuwafahamisha wengine kuhusu hotuba hiyo, kwa sababu ina ukweli mwingi ndani yake kwa wale wenye kuutafuta na kuusaka ukweli.

Related Articles

Leave a Reply

Check Also
Close
Back to top button
×