Habari za Bonyad

Bonyad Akhtar Taban ikisimamia majlis ya khitma na Ukumbusho wa kifo cha marhum Al-Haj Murtaza Ramzan Ali Karbala

Kikao cha Ibada ya Khitma na kumbukumbu ya kufariki kwa mtu huyu asiyechoka na msaidizi mkubwa wa marhum Allamah Rizvi (ra) kilisimamiwa na Bonyad Akhtar Taban.
Wageni walio hudhuria katika kikao hiki ni Waheshimiwa wakubwa na wanafunzi wa nchi za Bara la Afrika na India, pamoja na raisi wa Umoja wa Wanafunzi wa Afrika Mashariki, kilichofanyika katika ofisi za Bonyad Akhtar Taban zilizopo mjini Qom. Kikao hiki kilianza kwa kisomo cha Qur’ani Tukufu na kuendelea na hotuba ya mmoja wa wanazuoni wakubwa wa Jamuhuri ya kiislamu ya Iran akifahamika kwa jina la Hujjatul Islam wal-muslimiin Sheikh Nazari Munfarid na kisha baadae alizungumza mmoja wa wanazuoni wakubwa wa Afrika Mashariki Hujjatul Islam wal-muslimiin Sheikh Haidar Ali. Katika kikao hiki pia alihudhuria Hujjatul-Islam wal-muslimiin Bwana Syed Kazim Rizvi mjukuu wa marhum Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, juhudi zake na kujitolea kwake kwa ajili ya usaidizi wa marhum Allamah Rizvi (ra) bali zaidi ukaribu wake alionao kwa marhum Allamah (ra) ni jambo linalothaminiwa, kikao hiki kilihitimishwa kwa kisomo cha suratul Fatiha kwa ajili ya roho za wote waliohudumia Madhehebu ya Kishia.

Leave a Reply

Back to top button
×