Kuwakirimu na kuwapongeza Watangazaji washirika wa Lugha ya Kiswahili katika kuzalisha Mradi wa Podcast (matangazo ya kimitandao) ya Kiswahili

Buniyad Akhtar Taban iliwakirimu na kuwapongeza Watangazaji ambao walishiriki katika kipindi cha kuzalisha podcast (matangazo ya kimitandao) ya kitabu cha Marhum Allamah Sayyid Saed Akhtar Rizvi (r.a). Katika Mwaliko huu wa washiriki wa Mradi huu watangazaji wa Lugha ya Kiswahili walipongezwa kwa kupewa pesa keshi.
Katika kikao hiki ambacho kilifanyika katika Ofisi ya Buniyad Akhtar Taban Wageni Waswahili walionesha utayari wao wa kufanya Mradi mwingine  na walitangaza kuvutiwa kwao na ratiba hii  na walibainisha kuwa kulingana na mahitaji ya kizazi cha vijana kwenye mambo haya na ili kufaidika watu wote na zana za kisasa, Uandaliwe Mpango sahihi kwa ajili ya kufaidika vijana na watu wote na Tungo na Vitabu vya  Marhum Allamah Rizvi (r.a).

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button
×