Habari

Kufanyika kwa kumbukumbu ya kumi na tisa ya kifo cha Raisul Muballeghin Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (r.a) katika Husseiniyah ya Imam Swadiq (a.s)

Kikao hiki cha kumbukumbu ya kifo cha Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (r.a) kilifanyika Mji mtukufu wa Qom katika siku aliokufa, chini ya usimamizi wa Ofisi ya Bonyad Akhtar Taban.
Kikao hiki kilichofanyika katika Husseiniyah ya Imama Swadiq (a.s) kilihudhuriwa na Maulamaa na wanafunzi kutoka Bara la India.
Baada ya kisomo cha Qur’an kilichosomwa na msomaji Mheshimiwa bwana Jaydi, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Firuz Abbas Khan alisoma Mashairi ya kuwasifu Ahlul-Bayt (a.s) katika kumsifu Allamah (r.a).
Katika kikao hiki Khutuba ilitolewa na Sayyid Sibtain Abbas (M’ Mungu amuhifadhi) mmoja wa Walimu na Khatibu wa Hawza ya Qom Iran.
Katika Khutuba yake alielezea na kufafanua Daraja la A’lim na Tabligh ya Dini katika Hadith za Kiislam  na akaelezea pia Daraja la elimu na Shakhsia ya Allamah(r.a),  na alimalizia Khutuba yake kwa kuyakumbuka mateso ya Ahlul-Bayt (a.s).

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button
×