Habari

Tunawapongeza Waislamu wote duniani kwa kuadhimisha Siku adhimu ya Eid al-Mab’ath

Madhumuni ya ujumbe wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kutoka katika maneno ya Hadhrat Abu Talib (a.s)

Madhumuni ya ujumbe wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kutoka katika maneno ya Hadhrat Abu Talib (a.s).
Imepokewa kutoka kwa Abu Ra’fii kwamba anasema:

Abu Talib (a.s.) alikuwa akisema:
Nilimsikia mpwa wangu Muhammad bin Abdillah akisema kuwa Mola wake Mlezi amemtuma ili kuimarisha mafungamano baina ya jamaa zake (watu wake wa karibu) na wamuabudu Mwenyezi Mungu pekee, na wasimwabudu yeyote pamoja Naye, na Muhammad pia ni mkweli na mwaminifu. (Ibn Hajar, Al-Isabah Fi Tamyiz Al-Sahabah: 4/116).
Imetajwa pia katika nukuu kama hizo kwamba Hadhrat Abu Talib (AS) alisema:
“Mpwa wangu ambaye ni mwaminifu na msema kweli, ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba hakika yeye ni msema kweli sana, alinifahamisha kwamba Mola wake Mlezi amemtuma ili kuimarisha mafungamano baina ya jamaa (ndugu zake wa karibu), na kuswali na kutoa zaka”. (Al-Ghadir fi Al-Kitab wa al-Sunnah wa al-Adab, Juzuu ya 7, uk. 494).
Tunawapongeza Waislamu wote duniani kwa mnasaba wa Eid al-Mab’ath.

Related Articles

Leave a Reply

Check Also
Close
Back to top button
×