Habari za Bonyad

Kifo cha Ayatollah Seyyed Mohammad Sadiq Rouhani (RA)

Katika kipindi hichi cha maombolezo ya Hadhrat Fatima Zahra (sa), kimetokea kifo cha Ayatullah Sayyid Mohammad Sadiq Rouhani(ra) amvacho kimesababisha huzuni maradufu.

Tunatoa rambirambi zetu za dhati kwa kuondokewa na Mwana wa chuoni huyu Mcha-Mungu na mwenye maadili matukufu na kazi na huduma mbalimbali za kidini, kisayansi na kitamaduni na ambaye katika uhai wake alihudumu katika kumtumikia Hadhrat Waliyyu Asri (atf). Pia rambirambi hizi zimfikie Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Watoto na Manusura wa Marehemu, Waheshimiwa Maayatollah, Maulamaa, Wanazuoni, na Waheshimiwa Wanafunzi. Na tunamuombea dua njema Marehemu Allah amuweke katika Daraja za Juu.

17/12/2022

Leave a Reply

Back to top button
×